Special TTU Song(Swahili)
1. Chama cha Walimu, Tanzania moto moto.
Chama cha Walimu, Tanzania CWT.
Hulinda haki na Maslahi ya Walimu Nchini.
Husimamia Maadili mema ya Walimu Tanzania
Chama chetu Imara tena ni thabiti
Kiitikio
(Tuungane) Tuungane walimu wote nchini tuungane x 2
Mshikamano daima x 2
Mshikamano walimu ni Mkombozi wetu
Tufanye kazi kwa moyo x 2
Tufanye kazi kwa moyo, tujenge Taifa letu la Tanzania x2
2. Chama cha Walimu ni dira ya Walimu
Moto wetu wa Chama ni WAJIBU NA HAKI
Ni kiungo cha Walimu wote nchini Tanzania
Husuluhisha migogoro yote ya Walimu nchini
Husuluhisha migogoro yote ya Walimu nchini
Chama chetu Imara tena ni thabiti
Kiitikio
3. Chama cha Walimu Nchini Tanzania
Ni chama Imara na chenye Msimamo
Kinajenga Mahusiano mema na Vyama vingine
Kinashirikiana na vyama ndani na nje
Chama chetu Imara tena ni thabiti
Kiitikio