TAARIFA YA VITAMBULISHO VIPYA VYA WANACHAMA

Chama cha walimu Tanzania kupitia kitengo cha TEHAMA kimeanza kutoa vitambulisho vipya vya wanachama ambavyo vitawawezesha wanachama kupata huduma mbalimbali za chama nchi nzima kutumia kitambulisho cha aina moja.

kwa kuwa zoezi hili linaendeshwa na chama chenyewe faida zifuatazo zitapatikana
i. Gharama za utengenezaji vitambulisho zitapungua kwa asilimia sabini(70%) Kwa kuwa wastani wa gharama ya kitambulisho utakuwa Tsh. 2,800/= kwa kuzingatia bei ya malighafi kwa sasa ambapo Chama kitatumia wastani wa milioni mia sita sabini na mbili kutengeneza vitambulisho vya wanachama laki mbili na arobaini(240,000) waliopo ukilinganisha na wastani wa TSH 10,000/= kwa kitambilisho kimoja kutoka Kwa wazabuni , maana yake Chama kingetumia wastani wa Tsh. bilioni mbili na milioni mia nne (2,400,000,000/=) kwa vitambulisho vya wanachama wote.

ii. Chama kitakuwa na kitambulisho cha aina moja kwa wanachama wote kikiwa na alama za kisasa za utambuzi wa uhalali wa kitambulisho husika.

iii.Kitambulisho hicho kitasaidia mwanachama kupata huduma za chama sehemu yoyote nchini ukizingatia kuwa taarifa za kitambulisho hicho zitakuwa zimeunganishwa na mfumo wa kutunza taarifa za wanachama (TTU MEMEBERS REGISTRATION SYSTEM) ambapo namba zinazopatikana kwenye kitambulisho hicho zikiingizwa kwenye mfumo huo humwezesha mtoa huduma kupata taarifa muuhimu za mwanachama ikiwemo taarifa zake za ajira na taarifa mbalimbali za huduma ambazo mwanachama aliwahi kupatiwa.

iv Ni rahisi kutoa nakala ya kitambulisho kilichopotea kwa mwanachama kwa kuwa taarifa zote zitakuwa kwenye mfumo.

v.Kuendelea kuwa na uwiano wa usalama na uhalisia kwa kuwa vitambulisho vyote vinatolewa sehemu moja na alama za utambulisho wa usalama ni za aina moja.

Taarifa rasmi ya katibu mkuu wa CWT juu ya zoezi la Vitambulisho vipya vya wanachama

 


Taarifa rasmi ya katibu mkuu wa CWT juu ya zoezi la Vitambulisho vipya vya wanachama

 

Share:

Contact Info

  •  

    CWT DODOMA  HOUSE OPPOSITE JAMUHURI STADIUM DODOMA

  •  

    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…