Gender and Women teachers.

IDARA YA JINSIA NA WALIMU WANAWAKE

Contact Person: Mwl Mwandile Kiguhe  Title: Head of Department  Mobile: +255677520054 

Idara ya Jinsia na Walimu Wanawake ni miongoni mwa idara zilizopo Makao Makuu ya Chama cha Walimu Tanzania. Lengo kubwa la kuanzishwa kwa idara hii ni katika jitihada za Chama kuleta usawa wa kijinsia miongoni mwa wanachama wake, wanawake na wanaume. Mkuu wa Idara ndiye mshauri wa Katibu Mkuu katika masuala yanayohusiana na walimu wanawake katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Chama.

Kifungu cha 25 cha Katiba ya CWT kinatambua kuundwa na kuwepo kwa Kitengo cha Walimu Wanawake ambacho kitakuwa na Kamati za Jinsia na Walimu Wanawake. Kwa kuwa madhumuni (L) na (M) ya Katiba ya CWT yanazingatia kuundwa kwa sera madhubuti ya kulinda hadhi na haki za Walimu Wanawake dhidi ya bughudha za kijinsia, Chama kimeamua kuunda kamati za kushughulikia maendeleo na haki za Walimu Wanawake katika ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa.

 

MUUNDO WA KAMATI ZA JINSIA NA WALIMU WANAWAKE

 

Ngazi ya Wilaya

(i)      Mwenyekiti – Kamati  ya Jinsia na Walimu Wanawake Wilaya

(ii)     Katibu         -  Mwakilishi ‘Ke’ Wilaya

(iii)   Mweka Hazina     –  Kamati ya Jinsia na Walimu Wanawake Wilaya

(iv)  Wajumbe 4         -  Kamati ya Jinsia na Walimu Wanawake Wilaya

(v)    Katibu wa CWT Wilaya (Kwa wadhifa wake)

Ngazi ya Mkoa

(i)    Mwenyekiti      – Kamati ya Jinsia na Walimu Wanawake Mkoa

(ii)  Katibu             -  Mwakilishi ‘Ke’ Mkoa

(iii)Mweka Hazina –  Kamati ya Jinsia na Walimu Wanawake Mkoa

(iv)Wajumbe 3    -  Kamati ya Jinsia na Walimu Wanawake Mkoa

(v)  Katibu wa CWT Mkoa (Kwa wadhifa wake)

Ngazi ya Taifa

(i)      Mwenyekiti            -  Kamati ya Jinsia na Walimu Wanawake Taifa

(ii)    Katibu                            -  Mwakilishi ‘Ke’ Taifa

(iii)   Mweka Hazina        – Kamati ya Jinsia na Walimu Wanawake Taifa

(iv)  Mkuu wa Idara ya Jinsia na Walimu Wanawake

(v)    Mwakilishi mmoja toka kila Kanda ya CWT

(vi)  Wanawake walioko katika Kamati ya Utendaji ya Taifa

(vii)Mjumbe mmoja atakayechaguliwa toka miongoni mwa Wenyeviti wa Mikoa wa Kamati za Jinsia na Walimu Wanawake

(viii)Katibu Mkuu wa CWT (Kwa wadhifa wake)

 WAJIBU WA KAMATI ZA JINSIA NA WALIMU WANAWAKE

 

 1. Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Jinsia na Walimu Wanawake ndani

ya CWT.

 

 1. Kuwahamasisha na kuwaelimisha Walimu Wanawake kujiunga na CWT.

 

 1. Kuwahamasisha Walimu Wanawake kutimiza wajibu wao kazini kwa mujibu

wa Kanuni na Sheria za kazi.

 

 1. Kuwahimiza na kuwatia moyo Walimu Wanawake kugombea na kushika

nafasi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya Chama.

 

 1. Kutetea haki na maslahi ya Walimu Wanawake katika sehemu za kazi.

 

 1. Kuandaa na kuratibu mafunzo kwa Walimu Wanawake yahusuyo sheria za

kazi, kanuni na mikataba ya hali bora za kazi ambayo inazingatia zaidi masuala ya Wanawake na Jinsia.

 

 1. Kushirikiana na kushauriana na viongozi wengine wa Chama Cha Walimu

Tanzania na Waajiri kuchambua changamoto za Walimu Wanawake kisha

kubuni mbinu za utatuzi.

 

 1. Kukusanya, kuchambua, kujadili na kupanga program za Jinsia na Walimu Wanawake na kupeana taarifa zinazowahusu Walimu Wanawake.

 

 1. Kuwahimiza Walimu Wanawake wajiendeleze kitaaluma, kitaalamu,

kiuchumi na kushiriki katika vyombo mbalimbali vitoavyo maamuzi sehemu za kazi ndani ya CWT, serikalini, vyama vya siasa, taasisi na asasi zingine.

 

 1. Kutoa ushauri katika kutetea haki na masuala ya Jinsia na Walimu Wanawake katika migogoro na mikataba ya hali bora za kazi.
 1. Kuwahimiza waajiri kuanzisha huduma mbalimbali zitakazowawezesha

Walimu Wanawake kufanya kazi kwa ufanisi.  Kwa mfano vituo vya watoto

wadogo, sehemu za mapumziko, uzazi wa mpango na kujikinga na

UKIMWI.

 

 1. Kuwahimiza Walimu Wanawake kubuni, kuanzisha na kuendesha miradi

itakayowawezesha kuongeza kipato.

 1. Kuandaa majarida, vipindi vya redio na runinga, magazeti, tovuti na makala mbalimbali za Wanawake na Jinsia.

  

Current Updates